
Mkuki na Nyota Publishers
Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini

Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini
Kwa zaidi ya miaka kumi na tano vitabu vya mwandishi maarufu kushinda wote katika jamii za Waswahili kote Afrika ya Mashariki na Kati, Marehemu Sheikh Shaaban Robert, havikupatikana Tanzania. Sababu ya kukosekana kwa vitabu hivyo ni kuwa kampuni ya kigeni iliyovichapisha iliamua kuacha kuvichapisha kwa sababu haikulipwa kwa fedha za kigeni jambo, lililosabishwa na hali mbaya ya uchumi. Athari za kupotea kwa vitabu vya Sheikh Shaaban Robert katika miaka hiyo ni kwamba Watanzania wengi hasa wale wenye umri chini ya miaka thelathini, hawamjui mwandishi huyu maarufu na hawakulelewa katika mazingira ya utajiri wa maandishi yake ambayo bila shaka yoyote ni mfano pekee wa utajiri wa urithi wa utamaduni wetu. Kwa kuvichapisha vitabu vya Marehemeu Sheikh Shaaban Robert tunawakaribisha tena Watanzania, hasa vijana kuvisoma, kuburudishwa na kufunzwa na yale aliyoyaandika kwa sanaa na kipaji adimu.
An autobiographical work in poetry and prose.
Author: Shaaban Robert |
Publisher: Mkuki na Nyota Publishers |
Publication Date: Sep 07, 2018 |
Number of Pages: 138 pages |
Binding: Paperback or Softback |
ISBN-10: 9976973160 |
ISBN-13: 9789976973167 |