Skip to main content

Mkuki na Nyota Publishers

Kufa na Kupona

No reviews yet
Product Code: 9789987083138
ISBN13: 9789987083138
Condition: New
$24.49

Kufa na Kupona

$24.49
 

Nyaraka za siri zimeibiwa kutoka osi moja ya wapigania uhuru jijini Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania inaingiwa na hofu kuwa nyaraka hizo zitaishia mikononi mwa adui na kuhatarisha maisha ya watu wengi wasio na hatia.

Kutokana na ishara maalumu inasadikiwa kuwa majasusi hao wamekimbilia jijini Nairobi. Mpelelezi nguli, Willy Gamba, anapewa kazi ya kuwatafuta popote walipo, kwa gharama yoyote na kuwapokonya nyaraka hizo. Kazi hiyo lazima ifanyike haraka kabla hawajaziuza kwa adui.

Muda unazidi kwenda na mapambano ya kuwasaka majasusi hao yanazidi kuwa makali na hakuna huruma. Pande zote zinapoteza watu muhimu. Wapelelezi, majasusi na raia wengine wasio na hatia wanauwawa.

Wakati wote huo Willy Gamba anaendelea na upelelezi wake mgumu na ndipo anapokutana na mrembo Lina. Lakini mrembo huyu yuko upande gani? Na Lulu je? Je Chifu yupo sahihi anapomwonya Willy Gamba asimwamini mwanamke yeyote mrembo?

Willy Gamba na wenzake wanabanwa vilivyo lakini hawana ruhusa ya kushindwa. Maisha ya wengi yanawategemea. Ni mapambano ya kufa na kupona, lakini wanawashindaje maadui wakali kama hawa?

The four books in this series of detective novels, written in Swahili, were authored by the late Aristablus Elvis Musiba. The novels follow the exploits of Willy Gamba, an elite special operations Tanzanian intelligence officer. Set in various locations in Africa Willy is dispatched to neutralise agents within the Apartheid Regime as well as saboteurs, who are out to destroy those involved with the liberation struggles being waged in Southern Africa.




Author: A. E. Musiba
Publisher: Mkuki na Nyota Publishers
Publication Date: Nov 19, 2018
Number of Pages: 118 pages
Binding: Paperback or Softback
ISBN-10: 9987083137
ISBN-13: 9789987083138
 

Customer Reviews

This product hasn't received any reviews yet. Be the first to review this product!

Faster Shipping

Delivery in 3-8 days

Easy Returns

14 days returns

Discount upto 30%

Monthly discount on books

Outstanding Customer Service

Support 24 hours a day